Search in This Blog

PENNY ATESWA NA MIMBA YA DIAMOND

Penny akiwa hospitali.
Imejulikana kwamba mimba anayotamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa amempachika mpenzi wake, Peniel Mungilwa ‘Penny’, inadaiwa kuanza kumtesa mtangazaji huyo wa DTV, Ijumaa Wikienda linashuka nayo.
Habari zisizokuwa na chenga kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa mrembo huyo, zilieleza kwamba kufuatia hali hiyo, Penny alikimbizwa kwenye Hospitali ya Regency, Dar wikiendi iliyopita kisha  akalazwa, akachomwa sindano na kutundikiwa dripu.
Diamond na Penny katika pozi.
Akizungumzia hali hiyo, Penny aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli alizidiwa usiku na alikimbizwa hospitali ambapo pamoja na mengine lakini kubwa vipimo vilionesha kuwa alikuwa na malaria.
Hata hivyo, habari tulizozipata wakati tunakwenda mitamboni zilieleza kuwa Penny aliruhusiwa kutoka hospitalini na anaendelea vizuri.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger