Search in This Blog

WASANII WA BONGO MOVIE WAINGIA MITINI KWENYE MAZISHI YA MSANII MWENZAO KIHIYO YALYOFANYIKA JANA JIONI KWENYE MAKABURI YA MWINYIMKUU MAGOMENI


 Jeneza la marehemu Kihiyo likipelekwa kaburini tayari kwa mazishi yake yaliyofanyika leo jioni makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.
Jeneza la marehemu Kihiyo likipelekwa kaburini tayari kwa mazishi yake yaliyofanyika leo jioni makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.

 Jeneza la marehemu Kihiyo likiwasili eneo la makaburini tayari kwa mazishi yake yaliyofanyika leo jioni makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.

 Kaburi la marehemu Kihiyo linavyoonekana kwa ndani.
 Mwili wa marehemu Kihiyo ukiwa ndani ya kaburi.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

UBAGUZI wa wasanii Tanzania umedhihirika leo baada ya kususia msiba wa msanii mwenzao Hassan Kihiyo aliyezikwa saa kumi za jioni katika makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni.
Msiba huo ulihudhuriwa na wasanii wachache, hasa wale wasiokuwa na majina makubwa, licha ya Kihiyo kujitoa mara kwa mara katika matatizo ya wasanii wengine Tanzania.

Kihiyo alifariki jana jioni katika Hospitali ya Wilaya Temeke alipokuwa amelazwa akipata matibabu na kupeleka huzuni kubwa kwa baadhi ya wasanii na mashabiki wanaomuunga mkono.

Mazishi ya msanii huyu hayakuwa na tofauti  na watu wengi, licha ya kucheza filamu kadhaa na kushiriki kutengeneza movie za wasanii wengine kwa namna moja ama nyingine. Kihiyo alicheza filamu zaidi ya nne, ikiwamo ile Mother House, Kaburi Moja, Chanzo ni Mama, Where is God, My Book na nyinginezo.

Wadau na wasanii wachache waliohudhuria msiba huo ni pamoja na Emmanuel Shija, John Mtitu, John Lister, mtunzi wa filamu na maigizo Tanzania, Muddy Kimindu Kulinyangwa ambaye pia ametunga nyimbo mbalimbali za taarabu kama vile Domo la Udaku la T-Moto Taarab, Nani Kama Mama wa Isha Mashauzi na nyinginezo.

Mbali na kususia kwa wakali wa filamu Tanzania, mazishi ya Kihiyo yalifanyika vizuri na kutanguliwa na swala, ambapo msikiti haukuwa mbali na nyumbani ulipokuwapo msiba pamoja na sehemu ya makaburi aliyozikiwa marehemu.

Wasanii wa Tanzania kwa mtindo huo wameonekana kubaguana wenyewe kwa wenyewe, wakiangaliana usoni na wale wenye majina makubwa zaidi ndio wanaoishi kwa kujuliana hali, hasa katika matukio ya misiba wakiamini vyombo vya habari, wadau na mashabiki wataendelea kujazana kwa ajili ya kutaka kuuza sura.


 
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger