Rais Obama amewasili Afrika Kuisini jana kwa ziara ya siku tatu akitokea Senegal.
Watu hao wamekamatwa baada ya kudaiwa kuishi kinyume cha sheria Afrika Kusini. Baada ya Watanzania hao kutiwa mbaroni na vyombo vya usalama wamehifadhiwa hapa nchini kusubiri hatua za kisheria zaidi.
Ofisa mmoja wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Sadiki Msele amesema Watanzania hao walirejeshwa nchini jana na kwamba hivi sasa wanasubiri sheria kuchukua mkondo wake.
“Safisha safisha kama iliofanyika jijini Dar es Salaam, pia imefanyika Afrika Kusini na kuwaathiri wafanyabiashara na watu wengine,” amesema ofisa huyo.
Hivi sasa Rais Obama yupo Afrika Kusini akiwa ameongoza na mkewe Michelle Obama na watoto wao wawili; Malia na Sasha.
Kesho Rais Obama na ujumbe wake anatarajiwa kutua Tanzania kwa ziara ya siku mbili na Jumanne ataondoka kurejea Marekani.