Baada ya kujinyakulia tuzo ya msanii bora wa kike kutoka Zanzibar
International Film Festival 2013 (ZIFF) kupitia filamu ya woman of
principle, Elizabeth Michael aka Lulu anatarajia kuja na filamu yake
mpya itakayoitwa “foolish age”.
Kupitia filamu ya woman of principle, Lulu alijiongezea umaarufu na
kuonyesha uwezo mkubwa wa kushirikiana na mastaa wa kubwa kama Ray na
Nargis. Foolish age itajaa mastaa mbalimbali wenye uwezo mkubwa wa bongo
movie.
Lulu bado ajafunguka sana kuhusiana na location ya foolish age wala tarehe itakayo dondoka sokoni.