KUFUATIA Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa Filamu za Kibongo, Wema
Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au maarufu kama Madam amebadilika na kuondoa
vitu vyote visivyo vya asili mwilini mwake.
Wema alitupia picha yake kwenye mtandao wa kijamii akionekana amekata
nywele zote huku akiwa ameondoa kope za bandia na kutoa kucha
alizobandika kuashiria kuuheshimu mwezi huu huku akibaki na kila kitu
cha asili yake.
“Mwezi Mtukufu ni wa kuheshimiwa na kuweka kila
kitu pembeni, nafurahi kuwa hivi kwa maana hata kama nikifunga swala
zangu zitapokelewa vizuri,” alisema Wema.