Search in This Blog

FILAMU BONGO ALIYENUSURIKA KUFA KATIKA AJALI YA GARI


STAA wa filamu Bongo,Jacqueline Pentzel amesema amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari hivi karibuni.

Akizungumza na mwandishi wetu, Jacqueline alisema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbezi alipokuwa akielekea nyumbani kwa mama yake, Mbezi jijini Dar akiwa kwenye gari lake dogo, aliligonga kwa nyuma gari aina ya DCM.

“Ni ajali ya ajabu kweli niliipata, maana DCM limefunga breki za ghafla mbele yangu na mimi nilikuwa nimejisahau nikalivaa ila namshukuru Mungu kwa kuwa sijaumia ila gari langu tu ndiyo limeharibika vibaya kwenye shoo ya mbele,” alisema Jacqueline.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger