MTU AMBAYE HAJAWAHI KUOGA WALA KUKATA NYWELE KWA MIAKA 37 SASA.
Mr Singh na Mkewe
Hakika haya tunaweza kuyaita mafanikio ya ajabu kwa mzee huyu kutokana
maamuzi yake.Labda tumite Mr Adui wa Maji ila jina lake kamili ni Mr
Kailash Singh akiwa na ndiye anayeshikilia rekodi ya mtu anayenuka zaidi
kutokana na kutokuoga kwa zaidi ya miaka 37 sasa. Mr Singh, 65, hajaoga na hata kukata nywele zake zenye urefu wa futi 6 toka mwaka 1974, mda mfupi mara baada ya kutoka kuoa.
Akielezea juu ya uamuzi wake wakushangaza, Mr Singh anasema mchungaji alimuahidi zawadi ya mtoto wa kiume kama atafata ushauri.
Licha
ya majirani kuwa wanamtania na kumdhihaki jamaa huyo walishindwa
kubadili maamuzi yake na namna ya kipekee alifanikiwa kumshawishi mke
wake, ila cha ajabu zaidi ni pale ambapo imani yake imeonekana
kumdanganya kwani ameishia kupata watoto saba ambao wote ni wa kike.