Search in This Blog

DIWANI CCM AMBUTUA MKEWE, AMBAYE PIA NI DIWANI


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Diwani wa CCM wa Kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro, Injinia Edwin Chambo (62) amedaiwa kumshushia kichapo mkewe Imelda Chambo (50) na kusababisha kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Amani limetonywa.
Kwa mujibu wa mashuhuda, ugomvi huo ulichukua nafasi Alhamisi iliyopita saa 6 usiku nyumbani kwa wanandoa hao, Kihonda. Mke naye ni Diwani wa Kata ya Mkundi kwa ‘leseni’ ya CCM.
Inadaiwa kuwa, baada ya mheshimiwa diwani kumtwanga mkewe na kummwagisha damu, mke naye alichukua chupa ya bia na ‘kujirudishia’’, wote wakawa chapachapa kwa damu.
Siku ya tukio, paparazi wetu alipofika nyumbani kwa wanandoa hao alikuta tayari wameshakimbizwa hospitalini ndipo alielezwa kuwa chanzo cha ugomvi wao ni wivu wa mapenzi.
Paparazi wetu alitinga hospitali ya mkoa na kumkuta mke wa diwani huyo akiwa hoi kwenye wadi namba tatu.
Akizungumza kwa tabu na gazeti hili, Diwani Imelda alisema ndoa yao imedumu kwa miaka 30 na kubahatika kuzaa watoto watatu. “Naweza kusema nusu ya maisha yetu ya ndoa ni migogoro na mapigano.
“Ugomvi wa leo hauna kichwa wala miguu, nimerudi nyumbani nikaingia chumbani kwangu, yeye akanifuata na kugonga mlango, nilivyogoma kumfungulia akaenda kuchukua tofali la ‘Fatuma’ na kuja kuuvunja, akaingia ndani na kuanza kunipiga mateke kichwani. Picha za X-ray hizo hapo.
“Na mimi katika hali ya kujitetea nilisogea na kuchukua chupa ya bia nikaipiga chini ikapasuka na sehemu ya kipande chenye ncha kali nikamchoma nacho, akaanguka chini, ndipo nikapata nafasi ya kukimbia nje.
“Majirani walituchukua na kutuleta hapa hospitali mimi nimelazwa hapa wadi ya wanawake, yeye wadi ya wanaume.”
Amani lilifika wadi ya wanaume lakini halikumkuta Diwani Chambo huku kukiwa na habari kwamba amekwenda kutibiwa kwenye hospitali binafsi. Juhudi za kumsaka kwenye hospitali binafsi hazikufua dafu.
Wakati tunakwenda mitamboni, diwani huyo alipatikana na alipoulizwa alikiri kutokea kwa tukio hilo huku akigoma kwenda ndani zaidi akisema ni mambo ya kifamilia.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger