Search in This Blog

TRENI YA ABIRIA YAPATA AJALI ALFAJIRI YA LEO, YASITISHA KWA KUTOTOA HUDUMA.

ABIRIA WAKIPANDA KATIKA TRENI YA ABIRIA KATIKA STESHENI YA MOROGORO WAKATI WAKIELEKEA DAR ES SALAAM.WASAFIRI WA SHIRIKA LA RELI NCHINI (TRC) WAKIFURAHIA KUONDOKA KATIKA STESHENI YA MOROGORO BAADA YA KUKWAMA KWA MASAA TISA KUANZIA SAA 7:45 USIKU SEPTEMBA 19/2012 KUFUATIA INJINI YA TRENI ILIYOWASAFIRISHA KUTOKA MIKOA YA BARA KUHAMISHIWA KATIKA TRENI ILIYOKUWA IKITOKEA JIJINI DAR ES SALAAM KWENDA MIKOA YA BARA KUWA NA HITILAFU  KATIKA INJINI AMBAPO WALIONDOKA MKOANI MOROGORO MAJIRA YA SAA 4 ASUBUHI JUZI Friday, September 21, 2012.

PICHA YA MAKTABA WWW.JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM

.

LEO mnamo saa 11:30 asubuhi vichwa viwili vya treni ya huduma la jiji la Dar es Salaam vilipata ajali ya kugongwa na roli la mizigo aina ya Fusso katika makutano ya reli na barabara ya Kawawa jijini Dar es salaam , katika jali hiyo dereva wa Fusso alifariki duniani papohapo hata hivyo Utingo wake alinusurika.

Hata hivyo vichwa hivyo vya treni vilipata mkosi tena wa ajali ambapo viligongwa na basi dogo la Daladala aina ya Isuzu katika makutano ya reli eneo la Kamata. 

Tukio hilo lilisababisha majeruhi kadhaa katika basi hilo la daladala ambapo majeruhi  wamelaz
wa katika Hospitali ya Taifa Muhimbil wakiwemo askari wawili Polisi kutoka Kikosi cha Reli  mmojawapo akiwa  mahututi.

Vichwa hivyo viifanikiwa kufika stehesheni kwa wakati na kuanza kutoa huduma ya usafiri wa treni jijini  kutoka Dar Stesheni kwenda Ubungo Maziwa hadi saa 5 asubuhi hata hivyo huduma ya leo  jioni Julai 01, 2013, imesogezwa mbele na itaanza saa 12 jioni badala ya saa 10:30 alasiri. 

mabadiliko haya yamebidi yafanyike   kufuatia Jiji la Dar es Salaam kuwa na hekaheka ya kumpokea Raisi wa Marekani Barack Obama.

Aidha uongozi wa  TRL unawataarifu wakazi wa jiji kuwa kesho Julai 02, 2013, huduma za treni ya jiji hazitakuwepo hadi keshokutwa Julai 03, 2013, ambapo zitaendelea kama kawaida.

Imtolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
 Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu.

Makao Makuu ya TRL
Dar es Salaam.
Julai 01, 2013.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger