Search in This Blog

JOHARI HATAKI KUTOKA NJE YA NYUMBA BAADA YA KUINGIA AIBU YA KUGOMANIA PENZI LA RAY

Muigizaji maarufu Blandina Chagula(Johari) anadaiwa kuishi kwa kujificha ficha baada ya hivi karibuni kumshushia makonde muigizaji mwenzake Chuchu Hans ambapo kisa kilidaiwa ni kugombea penzi la Vicent Kigosi(Ray). 

Inadaiwa Johari hataki hata kukutana na watu wake wa karibu wakiwemo wasanii wenzake. 

Chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers kilisema kuwa kwa sasa Johari hataki kabisa kuonana na watu wake wa karibu, hata mtaani amekuwa haonekani mara kwa mara, anawakwepa hata wasanii wenzake, hii ni kutokana na lile sakata lake na Chuchu...

Nae Johari alipoulizwa na mtandao huo juu ya sababu ya kujifungia ndani alisema: "Niko nyumbani, sitaki kutembea sana kwani niko na likizo fupi, halafu hata hili sakata langu na Chuchu bado halijapoa"
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger