Search in This Blog

YANGA WAFULIA, WASHINDWA KUWALIPIA KODI YA NYUMBA WACHEZAJI WAKE KAVUMBAGU NA TWITE

Didier Kavumbagu.
BEKI wa Yanga raia wa Rwanda, Mbuyu Twite amezidi kuandamwa na mikosi msimu huu, baada ya sasa kubainika wakati wowote anaweza kufukuzwa katika nyumba aliyopanga kutokana na kushindwa kulipa kodi.
Taarifa ambazo, Championi Ijumaa imezipata kutoka kwa watu wa karibu na beki huyo mwenye asili ya DR Congo, ni kuwa yupo katika wakati mgumu kwa kuwa kodi ambayo alilipiwa na uongozi wa Yanga imeshamalizika na anatakiwa kulipa tena.
Chanzo cha habari kimeeleza kuwa nyumba hiyo iliyopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar, Mbuyu analipiwa kodi na uongozi wa klabu hiyo kwa mujibu wa mkataba wake, ambapo kwa mwezi anatakiwa kuilipia Sh 600,000, kodi ambayo inatakiwa kulipwa kwa mwaka mzima.
“Mbuyu ni kama amechanganyikiwa, kama unakumbuka hivi karibuni aliibiwa mara mbili, lakini sasa hili la kodi limekuja tena, kibaya zaidi ni tishio la wenye nyumba kutaka kumtimua kama ataendelea kusumbua kwa malipo, sijajua nini kitaendelea hapa ni jambo la kusubiri,” kilisema chanzo.
Wakati huohuo, taarifa za uhakika zinaeleza kuwa mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu naye pia yupo kwenye hali kama hiyo kwa kuwa kodi ya nyumba anayoishi Mikocheni jijini, imemalizika na bado haijalipwa.
Championi Ijumaa lilipomsaka Mbuyu, alishtushwa na taarifa hizo na kusema: “Umeambiwa na nani habari hizo? Tanzania hakuna siri, kweli nadaiwa kodi ya nyumba naomba ujue hivyo tu na tayari nimeshazungumza na viongozi wa klabu kulitatua hilo.”
Alipotafutwa Kavumbagu, hakupatikana mpaka tunaingia mitamboni.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger