Wanafunzi 58 wanusurika kifo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka.
Wanafunzi 58 wa shule ya sekondari ya Mmazami wilayani butiama mkoani Mara, wamelazazwa katika hospitali za Butiama na ya mkoa wa Mara mjini Musoma baada ya kupata ajali mbaya kufuatia gari walikuwa wakisafiria kutoka shuleni hapo kwenda shule ya sekondari ya Butuguri kwa shughuli za michezo kupinduka.
Majeruhi hao ni miongoni mwa wanafunzi 136 walikuwa wakisafiri kutumia gari aina ya fuso yenye namba za usajili T 737 AHR, ambayo inadaiwa kupinduka ndani ya kijiji cha Butuguri baada ya dereva wake Bw Francis Marwa kushindwa kuimudu kono mbaya ambayo iko katika barabara hiyo.
Daktari wa zamu wa hospitali ya butiama Dk. Gitera Nyange, amesema hospitali yake imepokea majeruhi 40 na wengine 18 kupelekwa hospitali ya mkoa na kati ya hao watatu walikuwa katika hali mbaya lakini madakatari wameweza kuokoa maisha ingawa mmoja walilazimika pia kupeleka hospitali ya musoma baada ya kugundua kuwa amevunjika paja la mguu wake wa kulia.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya butiama Bw Magina Magesa ambaye ametembelea majeruhi hao katika hospitali hizo kwajili ya kutoa pole kwa wanafunzi hao, amesema ingawa wanafunzi wengi wanaendelea vizuri lakini madaktari wameombwa kufanya uchunguzi wa kina na kuona wale wanahitaji kupelekwa hospitali ya rufaa ya Bugango jijini Mwanza wapelekwe mara moja.