Search in This Blog

MAITI YAKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA


Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la RAJAB KANDUNDA amekutwa akiwa amefariki katika nyumba moja kwenye chumba kinachomilikiwa na NASRI OMARI huku akiwa na dawa za kulevya tumboni katika eneo la Tabata jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam DCP SULEIMAN KOVA amesema jeshi hilo limepata taarifa za kuwepo kwa maiti hiyo kutoka kwa wasamaria wema na kufuatilia ambapo walifanikiwa kumtia mbaroni mmiliki wa chumba alipokutwa maiti huyo na mke wa marehemu.

Baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao maiti ya RAJAB KANDUNDA ambayo pia ilikutwa na pipi 33 za Heroin ilichukuliwa na polisi kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam ELIFADHIRI MGONJA ametumia fursa hiyo kuwataka watanzania kujikinga na ajali kabla hazijawapata ili kuepuka athari za kiuchumi zinazotokana na ajali za barabarani baada ya watu kufariki au kujeruhiwa na kupata ulemavu wa maisha ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya usalama barabarani.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger