Search in This Blog

MOURINHO- MATA JIFUNZE KUKABA UTACHEZA TU

London, England. Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amemtaka mchezaji wake kipenzi cha mashabiki Juan Mata kujifunza kukaba ili kujihakikishia namba katika kikosi chake.
Kiungo huyo alishinda tuzo ya mchezaji bora wa klabu hiyo wa mwaka kwa misimu miwili iliyopita, lakini tangu Mourinho ametua hapo amepoteza nafasi yake ndani ya Stamford Bridge.
“Sababu ya kwa nini kwa sasa hapati nafasi ya kucheza sana ni mambo nitakayozungumza naye si kuongea hadharani,” alisema Mreno huyo.
“Alicheza dhidi ya Everton tangu mwanzo wa mchezo na unaweza kuangalia uchezaji wake. Na aliingia akitokea benchi dhidi ya Basel wakati timu inaongoza bao 1-0 ... kipi kikubwa alichokifanya.
“Kitu kilichonifanya kumchezesha Ramires na Oscar karibu na wapinzani na Mata akiwa namba 10 nyuma ya mshambuliaji ili aweze kupitisha pasi za mwisho na kwa sababu najua ana kipaji kikubwa,” alisema Mourinho.
“Lakini kitu kingine ni lazima mchezaji azoee jinsi tunavyocheza.”
Chelsea walifungwa 1-0 na Everton katika ligi wiki iliyopita kabla ya kuchapwa 2-1 nyumbani na Basel ya Uswisi katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi E katika Ligi ya Mabingwa pale Jumatano.
Mata alikuwa kiungo tegemeo wa klabu hiyo msimu uliopita, lakini Mourinho ameonekana kupenda kumtumia zaidi Oscar kama kiungo mshambuliaji.
“Nataka kumfanya Oscar kuwa namba 10,” alisema kocha huyo wa zamani wa Real Madrid, Inter Milan na Porto.
“Nataka wachezaji wengine...kujifunza namna ya kucheza na vile walivyozoea kabla.
“Kama kuna mtu yeyote ataniambia Oscar hatokuwa mchezaji bora wa Chelsea msimu huu nitampiga vikali. Nataka kuwathibitishia mashabiki kwamba mimi ni bora
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger