Search in This Blog

PICHA MBALIMBALI ZIKIONYESHA WAKENYA WAKIOMBOLEZA

Baadhi ya Wakenya kutoka sehemu mbalimbali DMV wakiwa wamekusanyika kwa maombolezo ya mauaji yaliotokea jijini Nairobi siku ya Jumamosi Sept 21 ndani ya Westgate Mall jijini Nairobi Kenya.
Pastor Maurice Kinyanjui akifungua hafla hiyo kwa dua maalum ya maombolezo ya mauaji ya Westgate yaliofanyika mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial jJijini Washington, D.C.
Siyad Warsame Ali akisoma dua  maalum ya maombolezo ya mauaji ya Westgate yaliofanyika mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial jijini Washington, D.C jana.
Baadhi ya Wakenya wakiwa na huzuni wakati wa kuwakumbuka wenzao waliopoteza maisha Westgate.
Wanajumuiya wa Kenya DMV wakiwa na mishumaa ambayo ni ishara ya matumaini na upendo.
MC Humphrey One Mic Muturi akiwa mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial jijini Washington, D.C kwa ajili ya kuomboleza mauaji ya Westgate.
Baadhi ya Wakenya kutoka sehemu mbalimbali DMV wakiwasha mishumaa.
Mishumaa ya kuonyesha matumaini ya amani umoja na upendo kwa pamoja bila ya kujali itikadi ya aina yoyote.
 
Wakenya DMV wakiendelea na maombolezo.
Jumuiya ya Wakenya DMV wameomboleza mauaji yaliyotokea Westgate jijini Nairobi, ikiwa ni siku nane tangu kutokea kwa shambulio la kigaidi nchini Kenya, lililoua zaidi ya watu 67 na kujeruhi wasiopungua 175. Wakenya kutoka sehemu mbalimbali duniani wameungana na wenzao katika maombi na ishara za matumaini kwa wenzao wa nchini Kenya. Maombolezo hayo yalifanyika mbele ya jengo la Abraham Lincoln Memorial jijini Washington, D.C jana Jumapili.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger