Search in This Blog

AFARIKI DUNIA KWA KUKOSA HEWA, HII NI BAADA YA MLIPUKO

Mtu mmoja mkazi wa manispaa ya Morogoro amefariki dunia kwa kukosa hewa baada ya kutokea mlipuko katika tenki la lori la mafuta ya Petroli wakati akifanya matengenezo katika kituo cha mafuta cha Simba oil cha mjini Morogoro.
ITV imeshuhudia jitihada za jeshi la polisi na kikosi cha zimamoto na uokoaji wakishirikiana na wananchi katika kuondoa mwili wa marehemu ambapo wakizungumzia tukio hilo baadhi ya mashuhuda wamesema  marehemu alikuwa akichomelea vyuma ndani ya tenki hilo lililokuwa limeharibika ambapo gafla ulitokea mlipuko na kupelekea marehemu kukosa hewa ingawa  jitihada za kumtoa akiwa Hai zilishindikana kutokana na kukosa hewa.
Kwa upande wake mwakilishi wa zamu wa kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoa wa Morogoro Masoud Ramadhan amesema uchunguzi wa haraka uliofanyika umebaini  kuwa baada ya kutokea mlipuko uliosababishwa  harufu kali ya mafuta ndani ya tank hilo na ambapo mamehemu alikosa hewa 
Mwili wa marehemu umechukuliwa na jeshi la polisi na kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Morogoro.

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger