Search in This Blog

WANAFUNZI WA KIKE WAACHA SHULE SABABU YA MIMBA

WATOTO wa kike 1,056 wameacha masomo ya shule ya msingi kutokana na mimba zilizosababishwa na mazingira magumu wanayoishi zikiwamo tamaduni mbalimbali za makabila.

Takwimu hiyo ilitolewa jana na Mtaalamu wa Maendeleo ya Jamii, Rosely Kaihula wa Mfuko wa Maendeleo ya Watoto Ekama, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya mtoto wa kike duniani itakayoadhimishwa Oktoba 11, mwaka huu.

Mtaalamu huyo alisema sababu zingine ni mazingira magumu ikiwamo kutokuwa na kipato kwa wazazi ama walezi pindi mtoto anapohitaji mahitaji muhimu hali inayomsabaisha arubuniwe na hatimaye kujikuta na ujauzito.

Mratibu wa masuala ya Familia wa Shirika la SOS Children’s Villages, Magdalena George, alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa kwa jamii juu ya masuala mbalimbali yanayomsibu mtoto wa kike, na yataishirikisha serikali, watoto na NGO’s mbalimbali.

Maadhimisho ya mwaka huu ambayo yatafanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa na kuhutubiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Anna Maembe, yatakuwa na kaulimbiu inayosema: “Chochea ubunifu kuboresha elimu ya mtoto wa kike.”
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger