Search in This Blog

APIGWA HADI KUFA BAADA YA KUIBA MBAO

  
Kijana mmoja anaefahamika kwa jina la Boni amefariki dunia kutokana na kupigwa na wananchi wenye hasira baada ya kukutwa akiwa anaiba mbao ambazo zinatumika na mafundi kuwekea linter (linta)

Picha hii nikimuhoji Marehemu Boni kabla hajafariki dunia!

samahani picha zingine mtakazo ziona zinahitaji moyo!

Tukio hilo lililotokea Ijumaa saa 3 asubuhi maeneo ya nzasa eneo maarufu kama bonde la kwa Sanvu kijana huyo alikutwa na mkasa huo alipokua akijaribu kuiba mbao ambazo zilikua zinatumika na Mafundi kufungia linter kwenye nyumba ndipo alipo bambwa na mwenye nyumba hiyo ambae jina tunalihifadhi alipopiga kelele za kutaka msaada uliasababisha wananchi wakimbilie eneo la tukio.

wananchi hao wakaamua kuchukua sheria mkonononi licha ya kuonywa sana juu ya kuchukua sheria mikononi wakampiga, lakini kitu kilicho sababisha marehemu akutwe na maafa hayo ni kua alikamatwa eneo la katikati ambalo linagawanya maeneo mawili tofauti yani eneo la Nzasa na eneo la Maji matitu alivyokamatwa na wananchi wa nzasa walimpiga wakamuachia na kumwambia aondoke eneo hilo na asirudi tena wakati Marehemu anaondoka likatokea kundi kubwa la wananchi wa Maji matitu ambao walikua na hasira kwamba angalau leo wamempata mwizi anaewatobolea madirisha yao na mwizi wa vitu vyao kipigo kikaanza upya! ikabidi wananchi wa nzasa waanze tena kumuombea msamaha ili asije akafia maeneo ya kwao, kwa juhudi za wananchi wa nzasa walifanikiwa kuwatuliza wananchi wa Maji matitu ndipo mwandishi wa habari hizi alipo pata nafasi ya kumuhoji Boni je ni kweli ulikua umekuja kuiba?

Boni alilikiri mbele yangu kua kweli alifika eneo husika kwa ajili ya kuiba, ikabidi muandishi apige simu polisi ili wajwe wamchukue Bonikabla raia hawajaamua vingine wakati Marehemu Boni baada ya kuhakikishiwa kua hatapigwa tena na alijitahidi aondoke eneo hilo la tukio ndipo alipoishiwa nguvu na kudondoka kwenye choo kilichokua jirani na eneo hilo ambapo alikaa mpaka Asksri polisi walipofika lakini wakati wanataka kumuhoji Marehemu Boni alifariki dunia



                 Marehemu Boni akiwa amedondokea Chooni


                 

BONI AKIWA TAYARI AMEPATWA NA UMAUTI

Kijana huyo ambae Baba yake ni Askari Polisi na ni kijana anaetoka katika familia inayojiweza atazikwa leo huko maeneo ya Mbagala kwa wa mbili

Wananchi tuache kuchukua sheria mikonononi kwa kua pale yule anakua ni mtuhumiwa hakuna chombo chochote cha sheria ambacho kitakua kimemthibitisha kwamba ni muhalifu pia wewe ndie utakua umetenda kosa kubwa na lenye adhabu kubwa kuliko huyo unaemuhukumu mfano wa tukio hili Boni alitaka kuiba mbao wewe umeua! nani anaepaswa kushitakiwa na kufungwa?
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger