Dini inayoamini katika MUNGU lakini ikiruhusu yale ambayo
dini zingine zinapinga imeanzishwa eneo la mji mdogo wa Makongolosi
wilayani Chunya mkoani Mbeya,
Dini hiyo haiamini katika kutoa sadaka bali inasema
tunamtolea nani sadaka wakati Vitu vyote tulivyonavyo ni mali ya
MUNGU,kwa nini tunampa MUNGU mali zake Mwnyewe.!
Dini hiyo inaruhusu ulevi,uchawi na uzinzi kwa sababu
vimeumbwa na MUNGU,Vile vile inaamini hakuna dhambi duniani,Dini hiyo
inaitwa DIMAYO, sasa imeanza kuenezwa Mbeya