Search in This Blog

IGP MSATAAFU OMARI MAHITA HAJAPOOZA NA NI MZIMA WA AFYA

Mkuu wa jeshi la polisi mstaafu nchini

UVUMI uliozagaa juu ya Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi mstaafu Omary Mahita kuwa ni mgonjwa na amepooza upande mmoja si za kweli.Juhudi za kumtafuta na kuzungumza naye nyumbani kwake eneo la Forest kata ya Boma Manispaa ya Morogoro ambapo alishangazwa na uvumi huo na kusema kuwa hiyo ni mara ya pili kwa yeye kuvumishiwa hivyo. 

IGP mstaafu huyo ambaye amestaafu mwaka 2006, akizungumza na mwananshi wa habari hizi nyumba kwake alisema kuwa amekuwa akishangazwa na watu wanaomvumishia kuwa yeye ni mgonjwa na amepooza jambo ambalo si sahihi. 

“Nakumbuka mwaka 2006 nilivumishiwa kuwa naumwa sana, jambo la kushangaza mimi nilikuwa Arusha kikazi kwenye mambo ya TANAPA nikawa napigiwa simu ya kupewa pole nashangaa, sasa hii ni mara ya pili nimepigiwa sana simu za kupewa pole, sijui nani anavumisha hivyi,” alisema Mahita. 

Akizungumzia maisha yake ya sasa Mahita alisema kuwa kwa sasa ajishughulisha na  kilimo katika eneo la Dakawa wilayani Mvomero na amekuwa akilima mazao ya Mpunga, Mahindi na Alizeti.

Alipoulizwa juu ya kuwa na wazo la kugombea nafasi yeyote katika vyama vya siasa aliendelea kukana kuwa hana mpango wa kugombea nafasi yeyote, na kama uvumi huo unatokana na hisia hizo hao wanaofanya hivyo wajipotezea muda.

“Ndugu mwandishi hapa unapoona najiandaa kwenda zangu shambani kupeleka vifaa vya kilimo kwa vijana wangu, kama kuna mtu anafikiria kuwa mimi nataka nafasi yeyote sina mpango huo, najishugulisha na kilimo tu,”alisema IGP huyo mstaafu wa polisi.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger