Search in This Blog

KANISA LAUNGUZWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO BUGURUNI

WATU wasiojulikana jana wamelichoma moto kanisa la Baptist la Buguruni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 8:20 usiku.
Kamanda Minangi alisema kuwa mchungaji wa kanisa hilo ambaye anaishi jirani na eneo hilo la kanisa, alibaini kuwepo kwa moto huo baada ya kuona vitambaa vya madhabahu vikishika moto.
Alisema kuwa mchungaji pamoja na majirani walisaidiana kuuzima moto huo ambao ulianza kutanda mbele na kuunguza vitambaa.
“Ni kweli tukio hilo limetokea na hadi sasa tunaendelea na uchunguzi. Hakuna mtu ambaye amejeruhiwa,” alisema.
Kamanda alisema kuwa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ingawa polisi walipofanya upekuzi wa awali walipata kiberiti kilichoonekana kutelekezwa karibu na madhabahu hiyo.
Alisema kuwa kanisa hilo ambalo halijaisha, limejengwa juu na huku chini likiwa halijaisha limezungushiwa mabati.
“Moto huo haukuleta madhara makubwa na hata vilivyoungua ni vitambaa tu vile vinavyopambwa mbele ya madhabahu ambavyo ni vya nailoni,” alisema.

-Tanzania Daima
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger