Search in This Blog

"MAC 2 B AMEFARIKI DUNIA KWA SABABU YA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA." ......BABA MZAZI


MAREHEMU MAC 2 B WA KWANZA KUSHOTO AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KUNDI ZIMA LA WATEULE ENZI ZA UHAI WAKE.

Baba wa msanii MacMalick katikati akihojiwa.

 
BABA Mzazi wa marehemu MacMalick ambaye alikuwa msanii wa kundi la Wateule, Mzee Said Mohamed ames
ema kuwa matumizi ya madawa ya kulevya ni janga la Taifa.
Mzee huyo alisema kuwa kipindi ambacho mtoto wake anatumia madawa ya kulevya hakujua mapema na pale alipokuja kugundua anasema kuwa ilikuwa ni 'too late'.

Mzee huyo alisema kuwa madawa ya kulevya ni vita ya jamii nzima na si kuilaumu Serikali, “watu wanapenda kupata pesa za haraka, na pia watu wanapenda kuwalaumu wazazi kuchangia kwenye madawa ya kulevya kwa kuwadekeza watoto lakini si kweli”, alisema Mzee.

Baba alieleza kuwa kama mzazi hakufurahia hali hiyo na alitumia sehemu ya pato lake kumhudumia na kumsaidia hadi pale Mwenyezi Mungu alipomchukua.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger