Search in This Blog

"MIMI NIMETOBOA MASIKIO LAKINI MWAMNANGU HATOBOI NG'O"......BENNY KINYAIYA


MAMBO vipi msomaji wangu wa safu ya Staa na Mwana? Kama kawa hapa nakuletea maisha halisi mastaa wanavyoishi na watoto wao nyumbani.
Leo tunaye mtangazaji machachari wa Kipindi cha Mama Land, kinachorushwa kupitia Televisheni ya Clouds, Benny Kinyaiya ambaye ni baba wa mtoto mmoja aliyempa jina la Benny Kinyainya John Junior ambaye ana umri wa mwaka mmoja.
Benny anaishi na mwanaye nyumbani kwao Vijana Kinondoni, jijini Dar. Ili kumjua zaidi, shuka na makala haya:
Staa na Mwana: Mambo vipi Benny?
Kinyaiya: Safi tu karibu sana nyumbani.
Staa na Mwana: Umenishtua kweli, kumbe una mtoto? Nilikuwa sijui.
Kinyaiya: Hahaha! Mjini hapa, watu hawaaniki kila kitu hadharani. Kifupi nina mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja.
Staa na Mwana: Huoni kama umechelewa? Mbona umeshavumishiwa sana kuwa na totozi?
Kinyaiya: Hahahaha, si unajua tena unaweza kupitapita lakini usifanikiwe mara ghafla mambo yanajipa kama hivi.
Staa na Mwana: Uliyezaa naye anaitwa nani na je unaishi naye?
Kinyaiya: Jina kapuni bwana, siishi naye. Tunaweka mambo sawa kwanza.
Staa na Mwana: Ulijisikiaje kuitwa baba kwa mara ya kwanza?
Kinyaiya: Nilijisikia vizuri sana na nimejua hivi sasa nina majukumu.
Staa na Mwana: Nakuona umetoboa masikio yote sasa mtoto wako akikua na yeye akitaka kutoboa utamkubalia?
Kinyaiya: Mimi kwa kweli nataka kumlea mtoto wangu kwenye maadili mema.
Staa na Mwana: Kwani ulivyotoboa wewe, inamaanisha hauna maadili mema?
Kinyaiya: Hapana ila sitaki yeye afuate maisha yangu. Nataka yeye awe mwingine kabisa tofauti na mimi maana ujana ulikuwa mwingi sana.
Staa na Mwana: Umesema mama watoto wako huishi naye, sasa inakuwaje kuhusu malezi yako kwa mwanao?
Kinyaiya: Mara kwa mara huwa naenda kumuona mwanangu na ananijua vizuri sana hivyo atakuwa anayapata pindi ninapomtembelea.
Staa na Mwana: Nini ambacho unapenda mtoto wako afanye anapokuwa mkubwa?
Kinyaiya: Napenda aje kuwa mtangazaji kama mimi ila nitamsapoti kwa chochote atakachokichagua yeye.
 Staa na Mwana: Haya nakushukuru sana Kinyaiya.
Kinyaiya: Karibu tena nyumbani.

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger