Search in This Blog

MWANAMKE ABAKWA NA KUULIWA KIKATILI

Matukio ya kutisha na ya kikatili dhidi ya wanawake yamezidi kushika kasi America  kusini baada ya mwanamke mmoja anaye sadikiwa kuwa ni kijana kukutwa akiwa amekufa huku maiti yake ikiwa uchi wa mnyama katika mashamba ya wakulima wadogo wadogo huko Chalco Estados nchini Mexico.
Mashuhuda wa tukio hilo ambao ni wakulima walidai kuwa walikuta mwili wa mwanamke huyo ukiwa uchi huku mikono yake ikiwa imefungwa kwa kutumia ribbon,koo lake na pua yake vilikuwa vimekatwa kwa kutumia kitu chenye ncha kali.Pia mwili huo ulikutwa ukiwa na jeraha begani.

Wakisimulia tukio hilo wakulima hao walidai nguo za maiti huyo zilikuwa zimetupwa mita 1 kutoka eneo la tukio.
Baada ya kufanyika uchunguzi ndipo ilipo bainika kuwa mwanamke huyo ambae alitambuliwa kwa jina moja tu la victoria mwenye umri wa miaka 33 ni mkazi wa kijiji cha San Nicolás Tetelco.
Mamlaka husika ilidai kuwa kabla ya kuuawa victoria alibakwa na mtu aliye mbaka ni mwanakijiji mwenzake ambae aliamua kumuua akihofia kama angemuacha marehemu basi yeye ange kamatwa kutokana kitendo hicho cha kinyama
 

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger