STAA wa Majanga, Snura Antony Mushi ‘Snura’ amesema kamwe wanaume za
watu wasimmendee katika shoo zake kwani hakati mauno ili kuwapata hasa
wenye wake.
Akipiga stori na paparazi wetu, Snura alisema kukata
mauno kwenye shoo ndiyo silaha yake ya kuwateka mashabiki lakini
anashangaa kuona wanaume za watu ndiyo wanaongoza kwa kutuma maombi ya
kutongoza.
“Sipendi kabisa kusikia masuala ya wanaume za watu, siko
tayari kuvunja ndoa za watu. Pesa za kuhongwa sioni raha nazo hata
kidogo napenda za kujitafutia za kwangu,” alisema Snura.