NAY WA MITEGO ASWEKWA SERO BAADA YA KUTUMIA SARE ZA POLISI KUFANYIA VIDEO.
Rapper
Ney Wa Mitego ameniambia kuwa hii picha hapo juu tukio hilo limetokea
Jana wakati wana shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri kwa sasa
kwenye radio stations ' Salam Zao'. Ney
Wa Mitego Amesema ' Nikweli nilitupwa sero jana baada ya raia wasio
julikana kuleta fujo eneo la kazi yangu kwasababu kulikuwa na waigizaji
waliokuwa na sare za polisi. Watu hao sijuani nao na walijitambulisha
kama askari na kutaka kujua kwanini natumia sare za polisi kwenye video
yangu bila kibali. hicho ndio kitu kilichopelekea nikapelekwa polisi. Mitego
ameendela kusema kuwa baada ya kuka sero kwa dakika kama 15 mkuu wa
kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru baada ya
kutoa maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuonekana uraiani. Ney
aliwekwa sero Kwenye kituo cha polisi Urafiki kilichopo Manzese na wiki
ijayo video hii itaonekana kwenye vituo vya televison Tanzania.