Afisa
upelelezi wa wilaya Mbeya mtatiro akishukuru wakazi wa mtaa wa iyela
kwa ushirikiano utulivu waliouonyesha wakati wa zoezi la kutafuta
vidhibiti.
Kijana
Daniel Kossam (21) anatuhumiwa wa kumuua bosi wake Bi,Pelesi Chaula
(32)ambaye alikuwa akiishinaye nyumba moja huko mtaa wa Ilembo kata ya Iyela
mkoani mbeya
Daniel
alikuwa akiuza duka la vifaa vya pikipiki la bi, Pelesi lijulikanalo kwa
jina la 'Twiyanze' lililopo kijiji cha Mbalizi nje kidogo ya jiji la Mbeya.
Chanzo
cha ugonvi inadaiwa kuwa ni kuchelewa kurudi nyumbani kijana huyo ndipo Pelesi
alipochukua jukumu la kumuuliza jambo lililozua ugonvi katiyao na kusababisha
kifo cha bi.Pelesi Chaula.
Kifo
cha marehemu Pelesi kimetokana na kupigwa na kitu chenye ncha kali mwilini
mwake.
Wakati
mauaji hayo yanafanyika mume wa bi Pelesi Chaula alikuwa safarini wilayani
Makete mkoani Iringa.
Baada
ya mauaji hayo Kijana Daniel alichukua simu mbili za marehemu na simu yake
pamoja na fedha kiasi cha 114000/= na kuzitumbukiza chooni kisha alienda
kwa jirani kuwajulisha kuwa walikuwa wamevamiwa na majambazi na kwamba wamemuua
bosi wake huyo.
Majirani
walipofika eneo la tukio walishangaa kuona kuwa hakuana sehemu ya nyumba iliyokuwa
imevunjwa, walipo muuliza Daniel alijibu kuwa alisahau kufunga milango, baaada
ya majibu hayo waliingiwa na mashaka na kuamua kutoa taarifa polisi.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi Mjumbe wa serikali ya mtaa Bi,Neema Mwasampeta
alisema,' Dan alichelewa kurudi na alifokewa sana,nadhani hicho ndiyo
chanzo cha ugonvi wao'. aliongeza kuwa alimjua kijana huyo kwa muda wa mwaka
mmoja.
|