Wakati Wastara akitoa kauli hiyo,watu mbalimbali akiwemo mwanamke aliyewahi kukimbia penzi la jemba hilo, Lulu Semagongo maarufu kwa jina la (Anti Lulu), akidai kwamba jamaa anatabia ya kula nyuma na mbele tena kwa kulazisha na wakati mwingine anatumia hata dawa za kelevya kwa kumpa mwanamke, ili atimize hazma yake.
Akizungumza na Mdadisi Mambo Blog Anti Lulu alisema kwamba wakati akiwa kwenye mapenzi na Bond alishindwa kuvumilia ujinga wake na akalazimika kujiondokea kwa sababu si mwanaume mwenye maadili ya mapenzi.
"Huyo jamaa ni mbaya hafai hata kidogo mimi namwonea huruma sana Wastara maskini, asiposikilisha ushauri huu ataendelea kufanyishwa mapenzi sana kinyume na maumbele yake"alisema Anti Lulu na kuonge:;
"Minaona anampango wa kujichafualia sifa yake, najua watu wanaweza kusema kwamba nina mharibia, lakini ukweli ni kwamba jamaa nilimuacha kutokana na tabia hiyo, kitambo hivyo siwezi kuwa na wivu na Wastara, ila ninamshauri awe makini na huyo jamaa kwani ni nomaa sana mwanzo ukimuona utadhani kuwa ni mtu, lakini ukishaa kolea kwake utakoma, na kama anabisha asubiri kuona matokeo yake"alisema Anti Lulu kwa kujiamini.
Hata hivyo Wastara pamoja na jemba lake wamekuwa wakinukuliwa katika mitandao mbalimbali wakikana kuwa na mahusiano ya mapenzi, zaidi ya mahusiano ya kazi kwani hivi sasa wako katika hatua za mwisho za kuandaa filamu yao mpya, itakayojulikana kwa jina la 'Uaminifu Dhaifu' "sina mahusiano na Bond zaidi ya kikazi tu na zile picha zote ambazo unaziona ni wakati tupo location, tukiandaa filamu yake inayoitwa Uaminifu Dhaifu, huo ndiyo ukweli, bora mume wangu angekuwepo haya yote yasingetokea"alisema Wastars.
Naye Bond kwa uapnde wake alisema kwamba Anti Lulu ni muongo sana,"Sio kweli ni picha za kazi tu ambazo hata wewe nilikutumia magazeti yanazigeuza, Lulu achana nae anatafuta kuandikwa, tulishachana kitambo wala hatuna mawasiliano"alisema Band.