CHRIS
Brown ameamua kumaliza migogoro na majirani zake huko Los Angeles,
Marekani kwa kuamua kuiweka sokoni nyumba yake.Mwimbaji huyo wa kibao
kinachotamba cha ‘Kiss Kiss’ amekuwa katika mizozo mara kadhaa na
majirani zake katika kitongoji cha Hollywood Hills baada ya kufunika
ukuta wa nje ya nyumba yake na michoro ya graffiti.
Staa huyo aliamriwa kulipa faini ya dola 376 mwezi Mei kutokana na kutokuwa na kibali na kujaza michoro kibao ukutani, na sasa ameamua kufunga virago na kuondoka kwa kuuza nyumba yake hiyo dola milioni 1.5.
Habari zinapasha kuwa mpenzi huyo wa zamani wa Rihanna ana mpango wa kuhamishia makazi katika mji wa Malibu huko Los Angeles County katika Jimbo la California ambao kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2010 unakaliwa na watu 12,645.