DAKTARI wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Salha Hassan
amejikuta akipigwa talaka na mume wake, Abdullatif Mohamed kufuatia
picha zake chafu akiwa na mwanaume mwingine kunaswa kwenye simu yake
mkononi, Uwazi limenyetishiwa.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Abdul alisema alifunga ndoa na Salha Februari 15, 2007 na waliishi kwa upendo mkubwa.
KISA KILIPOANZIA
Abdul alisema kuwa mwaka 2010
mkewe aliondoka Zanzibar na kwenda kuongeza ujuzi kwenye Chuo Kikuu cha
Udaktari Muhimbili jijini Dar es Salaam.
MKE ALALAMIKIA SIMU YAKE MBOVU, AAHIDIWA KUNUNULIWA MPYA
“Akiwa pale Muhimbili mke wangu alinieleza kuwa simu yake ya mkononi
(Nokia) inamsumbua sana, nikamshauri kwamba akirudi huku tuiuze halafu
nimnunulie nyingine,” alisema Abdul.
Aliongeza kuwa, katika mwaka wa tatu, mkewe alipofanya mtihani
alifeli, hivyo akalazimika kurejea Zanzibar kuendelea na kazi katika
hospitali anayofanyia kazi.
SIMU MBOVU YAENDA SOKONI, MKE ATOA ‘MEMORY CARD’
“Siku kadhaa baada ya kurejea, nilichukua simu yake kwa lengo la kwenda
kuiuza kama tulivyokubaliana, lakini mke wangu alitoa ‘memory card’
yake ambayo najua mlikuwa na vikorokoro vyake, hilo sikulifuatilia.
“Tayari nilishapata mteja, tukakubaliana bei lakini kabla ya
kumkabidhi niliamua kufuta vitu vingine ambavyo vilikuwa ndani ya simu
ya mke wangu. Wewe mwandishi unajua, simu zina ‘dokumenti’ mbalimbali,”
alisema Abdul.
MAMBO HADHARANI
Abdul alisema kuwa akiwa katika
zoezi la kufuta kumbukumbu mbalimbali zilizokuwemo kwenye simu hiyo,
ghafla alizibamba picha chafu za mke wake akiwa na mwanaume mwingine
ambaye hakumjua.
“Nilishtuka sana, sikuwahi kufikiria. Hata hivyo, awali nilidhani
naota ndoto, lakini baadaye nikajiridhisha kwamba sikuwa ndotoni,”
alisema Abdul.
AANGUKA, AZIMIA
Mwanaume huyo aliongeza kwamba, kufuatia tukio hilo baya machoni mwake alijikuta akianguka na kupoteza fahamu.
MTAZAMO WA PICHA
Abdul alimuonesha paparazi wetu
picha alizozinasa ambapo moja, Salha anaonekana amelala kitandani akiwa
amenyoosha miguu kwa kujisitiri na ‘kufuli’ tu.
Picha nyingine amepozi kwa kuegemeana na mwanaume huyo ambaye Abdul
alisema anaamini anaishi jijini Dar es Salaam au alikuwa akisoma naye
Muhimbili.
Picha nyingine, Salha anaonekana amepozi katika mkao tata akiwa
mtupu. Picha mbili zilionesha alijipiga mwenyewe isipokuwa ile aliyolala
kitandani.
ASITISHA KUUZA SIMU
Abdul alisema kuwa kufuatia
kuuona uozo huo wa mke wake aliyempenda sana, baada ya kuzinduka
alibatilisha uamuzi wa kuiuza simu hiyo na kurejea nyumbani ambapo
alipomuuliza, mwanamke huyo hakuwa na majibu ya kujitosheleza.
Waligombana sana na mwishowe aliamua kumrudisha nyumbani kwa wazazi wake ‘akimsindikizia’ talaka juu kwamba si mke wake tena.
MUME ADAI MOYO ULISHINDWA KUVUMILIA
Akasema:
“Kwa kweli sikuweza kukivumilia kitendo kile, haikuwa nia yangu kumpa
talaka lakini moyo ulishindwa kuvumilia kuona mke wangu yupo kama
alivyozaliwa.
UWAZI LAMSAKA MKE, AUKANA UDAKTARI
Baada ya
kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Salha kwa njia ya simu
yake ya kiganjani (huenda alinunua simu nyingine au aliitengeneza
ileile) ambapo baada ya kumpata na kumsomea mashitaka yake kuhusu picha
hizo, alijibu kwa jeuri:
“Mimi naona ulizokuwa nazo (picha) hazikutoshi kabisa. Ninazo
nyingine, kama upo tayari nikutumie ili uziongezee kwenye habari yako.
Kwanza mimi siyo daktari.
Uwazi: Sikia Salha…
Salha akakata simu.
TAHADHARI
Uzoefu unaonesha kuwa, tangu simu za
mkononi zilipoingia nchini Tanzania, wapendanao, wakiwemo wachumba,
wamekuwa wakiingia kwenye migogoro mikubwa inayosababishwa na matumizi
mabaya ya simu hizo.
Ni vyema wapendanao wakachukua tahadhari kuhusu matumizi ya simu zao.
Baadhi ya wafuatiliaji wa masuala ya ndoa wanasema kuwa hakuna kiwango
cha juu cha wanandoa kutopendana kama usaliti.


