
Akizungumza na Bongo5 leo, John ambaye yupo jijini Arusha, alisema wamepata mawazo ya kufanya series ya comedy kutoka kwa watu mbalimbali kuwa wafanya vipindi vya kuchekesha.
“Sio kwamba mbio za muziki zimeshindikana, tuna nyimbo kama tatu ila tumeamua kufanya filamu pia kwa upande wa comedy na tayari tumeshaanza kuvichukua vipande vipande vya show yetu ya comedy ambayo itaonyeshwa kwenye TV,” amesema msanii huyo anayejulikana kwa mtindo wa kurap kilevi.
“Unajua wasanii wengi wamezoea kwenda kwenye filamu za kawaida na sio comedy, sasa wanashangaa kumuona Ras na John wanaingia kwenye comedy. hiki ni kitu cha kawaida tu ,kwasababu tupo huru kufanya chochote. Kwahiyo watu wasubirie kuona kama tunaweza kuchekesha ama hatuwezi.”