Search in This Blog

KIPA WA SIMBA DHAIRA KUTIMULIWA, SASA SIMBA WANATAFUNDA KIPA MZAWA

Zacharia Hans Poppe.
WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC wamewataka mashabiki wao kuwa watulivu wakati huu wa dirisha dogo la usajili kwani kamati iko makini kutafuta wachezaji makini kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo, kepteini wa zamani wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ), Zacharia Hans Poppe ameuambia mtandao huu kuwa kwa sasa wanahangaikia nafasi ya mlinda mlango na nia yao ni kusajili kipa mzawa kujiandaa na utarabu mpya utakaoanza kutumika mwakani.
“Kama utaratibu mpya utaanza kutumika mwakani ambapo nafasi za wachezaji wa kigeni ni tatu  tu na kipa lazima awe Mtanzania., lazima tutafute kipa mzawa ili kujiandaa na sheria hiyo mpya”. Alisema Poppe.
Poppe alisema tayari wameshapokea taarifa kutoka kamati ya ufundi na leo hii watapata maono yao baada ya hapo na wao kamati ya usajili wataingia kazini.
“Dirisha dogo tunahitaji wachezaji wawili au watatu ili kuongeza nguvu zaidi, tumeona wachezaji wengi wa kusajili, lakini tutaangalia maeneo muhimu zaidi kwa sasa ikiwemo nafasi ya mlinda mlango”. Aliongeza Poppe.
Kepteini huyo wa zamani wa JWTZ aliwataka mashabiki wa Simba kuwa na imani kubwa na viongozi wao kwani wanafanya kazi kwa weledi mkubwa kwa malengo ya kuifikisha klabu mbali zaidi.
“Wapo wachezaji wengi wa kuwasajii, lakini mashabiki na wanachama waelewe kuwa tunafanya kazi kuzingatia majukumu tuliyojipangia, hivyo watuamini sana”. Aliomba Poppe.
Mwishoni mwa mzunguko wa kwanza, baadhi ya mashabiki wa Simba na viongozi  walitaka kumrejesha aliyekuwa mlinda mlango wao Juma Kaseja Juma kwa madai kuwa kipa wao wa sasa, Mganda Abel Dhaira hana ubora wanaoutaka wao.
Dhaira amekuwa katika wakati mgumu kutokana na shinikizo la kutaka aondolewe, lakini kwa upande wake amekuwa akisisitizamkuwa yeye ni kipa bora na kama anafanya makosa ni ya kawaida sana katika soka.
Lakini wamemkosa Kaseja aliyeitumia Simba kwa miaka 10 na mwishoni mwa msimu uliopita alinyimwa mkatana mpya na kukosa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu kwani hakuwa na timu, ila kwa sasa ni jembe halali la Yanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la milioni 40 za Kitanzania.
Yanga SC wamemsajili Kaseja kutokana na uzoefu wake wa michuano ya kimataifa ikizingatiwa kuwa  mwkaani wao ndio  wawakilishi wa Tanzania  katika michuano mikubwa ya klabu bingwa  barani Afrika .
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger