Search in This Blog

WANAOWAFICHUA WACHAWI WAKAMATWA NA POLISI KWA KOSA LA KUWASAKA WACHAWI

Baadhi ya Wataalamu wa kufichua watu wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina na uchawi maarufu KAMCHAPE wamejikuta wakiwa kwenye mikono ya dola baada ya kuendesha zoezi la kufichua uchawi katika nyumba kadhaa kwenye vijiji mbalimbali vya manispaa ya Tabora ambapo baadhi ya wananchi walililalamikia zoezi hilo kwa madai kwamba limekuwa likiwadharirisha baadhi ya watu pamoja na kujenga chuki ambazo huenda zikasababisha madhara makubwa katika jamii.
Hapa ni baada ya kufikishwa kituo kikubwa cha Polisi mjini Tabora kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya ambapo aliwataka kuacha mara moja zoezi hilo la kufichua wachawi.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger