Search in This Blog

MATONYA ATEKWA USIKU WA MANANE AKIWA CLUB KIBO TEGETA, NA KUPORWA GARI LAKE

Mwanamuziki nyota wa muziki wa kizazi kipya usiku wa kuamkia Jumatatu alionja joto ya kiwe baada ya kutekwa na kusurubiwa kisha kunyang'anywa kila kitu pamoja na gari yake. Mdadisi Mambo blog inakupa mkasa kamili
Mwanamuziki huyo akiwa kwenye viunga vya Club ya usiku ya  Kibo iliyopo Tegeta Jijini Dar pamoja masisita du wakila bata ghafra kundi la watu watano lilimvamia na kumkamta msobe msobe hadi nje ya ukumbi pamoja na kumrukisha kichurachura huku wakina dada waliokuwa wamendamana nao wakilia kwa uchungu kwa kumuonea huruma.
Habari zaidi toka kwa chanzo chetu cha paparazi kilichoshuhudia timbwiri hilo kilisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kudaiwa kwa Matonya na mtoto wa mjini aliyefahamika kwa jina la  Evance" Huyu Evance ni mtoto wa mjini na huwa anawakopesha pesa wanamuziki mbalimbali pamoja na wasanii wa bongo movie hivyo miezi ya hivi karibuni alimkopesha shilingi laki nne msanii huyo kwa madai kuwa hakuwa na pesa ya kula bata wikiendi ambapo baada ya kumkopesha msanii alianza kuzungusha kurudisha hali iliyomfanya Evance kuchukua hatua za kumfanyia unyambilisi huo" Kilisema chanzo chetu

Hata hivyo baada ya kumkamata msanii huyo Evance alimpeleka Oysterbay ambapo aliiacha gari na simu kwa makubaliano atakapoleta pesa hiyo atapewa gari yake na simu.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger