Mwanzilishi wa show hiyo ambaye pia ni jaji mkuu, Rita Paulsen aka Madam Rita, amesema wameamua kufanya hivyo kwakuwa washindi wamekuwa wakizitumia fedha wanazopata kwa mambo mengine na kusahau muziki.
Ameongeza kuwa wameamua kufanya hivyo kuondoa lawama za watu kuwa washindi hupotea mapema.
"Tumegundua kwamba wasanii hawawezi kutumia hizo hela kujijenga. Wanaweza kutumia kwa vitu vingi ambavyo ni mahitaji pia sijui nyumba, gari," amewaambia waandishi wa habari leo.
"Management company inaleta proposal, tunatengeneza video kadhaa, tunatengeneza promotion ya wimbo wako. Kutakuwa na mwanasheria na yeye mwenyewe anaauthorise ile hela inaenda kufanya hivyo vitu."
Fainali ya shindano hilo itafanyika November 30, jijini Dar es Salaam.