Search in This Blog

NDOA YA MIKE, THEA YAVURUGIKA, KISA NI KUKOSEKANA UAMINIFU


Mike Sangu na Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ siku ya ndoa yao.

Ndoa ya mastaa wa filamu, Mike Sangu na Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ imevurugika baada ya kutokea hali ya kuzinguana kwa wawili hao chanzo kikidaiwa ni kukosekana uaminifu.

Chanzo cha habari hii ambacho ni rafiki wa Thea kilieleza kuwa, kutibuana kwa wanandoa hao kumekua kufuatia Thea kuhisi mwenzake anamzunguka.“Kimsingi hali si shwari, ndoa inawaka moto, Thea anamtuhumu Mike kuwa anamsaliti, chanzo ni hizi simu na siku hiyo mtiti ulipotokea, shosti alikwenda kwao na mpaka leo hii (Juzi Jumatato) anasubiri wasuluhishwe,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kupata taarifa hizo, Mike alitafutwa na alipoulizwa kuhusu ndoa yake kutibuka alisema: “Mh! Watu ni wambeya sana mimi na mke wangu tulitokea kutoelewana na si mambo ya meseji wala wanawake, mimi sina mambo hayo kabisa, siwezi kuongelea mambo mengi mpaka nitakapoenda nyumbani kwa mke wangu lakini kilichotokea ni cha kawaida tu .”Thea hakuweza kupatika kuzungumzia ishu hiyo.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger