*Aweka msimamo wake wazi
*Ashangazwa na Kagame, Museveni kuitenga Tanzania
*Atofautiana na Membe
RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa pamoja na vinavyofanywa na viongozi wa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ya kuitenga
Tanzania, katu haitajiondoa katika jumuiya hiyo.
Pamoja na hali hiyo, Rais Kikwete ameshangazwa na madai kutoka kwa
wanachama wa EAC ya kwamba Tanzania haina moyo wala dhamira ya dhati ya
kuendeleza utengamano wa Afrika Mashariki.
Kauli hiyo aliitoa jana mjini Dodoma, alipokuwa akihutubia Bunge ambapo
pamoja na mambo mengine alizungumzia hali ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC).
