Ray C: Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana
Ray C aliitumia siku hiyo kuungana na watu walioacha kutumia dawa za kulevya, na kwa pamoja walijipongeza kwa hatua hiyo.
Kupitia Instagram, juzi (November 8) Ray C alipost picha akiwa na watu hao na kuandika ujumbe kuonesha upendo wake kwao, na kwa kuona watu wanaweza kuacha kabisa matumizi ya dawa hizo anaamini Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana.
“@ Nawapenda sana hawa wenzangu wote tuligundua tatizo tukasaidiwa na sasa Tumepona na tunamshukuru Mungu....Tanzania bila Madawa ya Kulevya inawezekana.”
Baada ya kumaliza kupeana pongezi na elimu zaidi kuhusu athari za matumizi ya madawa ya kulevya, Ray C aliielezea siku hiyo kupitia Instagram.
“Looooong day but am very happy....8/11/2013 Will always remember ths special Day......God!I heart You....” aliandika Ray C