Khaleed Mohamed 'TID'.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohamed 'TID' yupo
mahabusu katika Kituo cha Polisi Oysterbay tangu jana usiku baada ya
kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi msichana
anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, Mariam Nnauye.