Wiki hii Nay wa Mitego alifanya
mahojiano marefu na mtangazaji wa kipindi cha Mambo Mseto (Radio
Citizen, Kenya) Willy M Tuva kuhusiana na mambo mengi kuanzia tofauti
zake na Chidi Benz, Madee na Kimbunga.
Nay wa Mitego akiwa na mtangazaji wa Radio Citizen, Willy M Tuva
Akijibu madai ya rapper Kimbunga kuwa
alikuwa amepanga kumshirikisha kwenye hit yake Salam Zao lakini baadaye
akamtosa, Nay alisema hakuwahi kumwambia kuwa angemshirikisha.
“Kimbunga ni mshkaji wangu, ni mtu ambaye hajielewi,” alisema Nay.
“Mimi sikuwahi kumwambia kwamba ‘nataka
kufanya collabo na wewe’ hata siku moja. Lakini sijui alikaa na akina
nani wakashikana masikio wakamwambia ‘bwana ukitaka kutoka pitia hapa’
akafanya hivyo. Mi sikuwa na time ya kujibizana naye, mimi niliendelea
kufanya yangu. Siwezi kufanya competition na mtu ambaye hayupo level
yangu.”
Akimuongelea Madee, Nay amesema kwanza
hakubaliani na taarifa kuwa hitmaker huyo wa ‘Sio Mimi’ ni miongoni mwa
wasanii wenye fedha nyingi.
“Ukisema Madee ni miongoni mwa wasanii
ambao wanaingiza fedha nyingi sana hicho kitu hakina uhakika. Madee
labda wimbo uliomuingizia hela ni ‘Nani Kamwaga Pombe Yangu’. Lakini
ukitaja wasanii ambao wana hela Bongo, ukimweka Madee umekosea sana.”
Hata hivyo Nay amesema ugomvi wake na Madee ni wa kibiashara na sio wa
kupigana.
Akiongelea ugomvi wake na Chidi Benz, Nay alisema kwa sasa tofauti zao hazipo tena.
“Ziliisha tofauti zetu kama miezi mitatu
hivi minne tulikuwa kwenye tour, tofauti ziliisha, yeye ndio alikuwa
ana tofauti na mimi lakini mimi always sipendagi kuwa na tofauti na mtu
ila nikiongea huwa naongea kitu cha ukweli. So this time tunaongea,
tunapigiana simu kila kitu kiko sawa.”