MASTAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka na
Wema Sepetu wanadaiwa kuingia vitani, mpambe mmoja wa Wema akitumia
mtandao wa kijamii wa Instagram alimtuhumu Rose kwamba aliwahi kushiriki
kikao kimoja kilichokuwa kikimjadili ‘madam’ huyo sanjari na kumtukana.
Mpambe huyo aliyetumia picha ya Wema
(huenda akawa Wema mwenyewe), alisema kuwa siku moja isiyokuwa na jina
hivi karibuni, Rose alishiriki kikao hicho kilichofanyika kwenye Viwanja
vya Leaders jijini Dar es Salaam ambapo sehemu kubwa ya mazungumzo
ilikuwa ikimchambua Wema.
Akizungumza na Amani kwa njia ya simu
juzi kuhusiana na tuhuma hizo, Rose alisema anashangaa matusi
anayotukanwa na mtu huyo kwani ana mwaka mmoja hajawahi kukanyaga
katikia viwanja hivyo vilivyopo Kinondoni, Dar.
“Kiukweli huyo mtu amenitukana bure,
hajakaa na kufanyia uchunguzi hizo taarifa alizopewa, mimi sikumbuki
kama kuna siku niliwahi kukaa Leaders na kuanza kumsema vibaya Wema
kwani nina mwaka sijawahi kufika Leaders.
“Binafsi sina muda huo wa kumzungumzia
mtu au kukaa na mtu ambaye hana faida kwangu. Mimi rafiki yangu ni
mchumba wangu (Malick Bandawe), mama yangu na ndugu zangu zaidi ya hapo
tunakutana shutingi tukimaliza narudi kwangu, namsihi huyo mpambe wa
Wema afanye tena uchunguzi,” alisema Rose.
Juzi, Amani lilimsaka Wema kwa njia ya
simu ya mkononi ili azungumzie madai hao lakini hakupatikana. Hata
hivyo, habari zinasema kuwa mtu aliyemtukana Rose kwenye mtandao
alitumwa na Wema au Wema mwenyewe.
Tangu Diamond kurudiana na Wema na
kusambaza picha zao katika mitandao ya kijamii, hivi karibuni Wema
kufiwa na baba yake mzazi (Isaac Sepetu) na baadhi ya wasanii wa Bongo
Muvi kususia msiba huo, kumeibuka makundi ya watu kazi yao kubwa ni
kutukana watu ambao wako tofauti na Wema.
