Search in This Blog

ATABIRI DIAMOND KUFULIA KIMUZIKI NA KIFEDHA, SOMA KUMJUA NI NANI HUYO MTABIRI

Mtu mmoja anayedai kuwa mganga aliyemtoa mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz ameibuka tena na kueleza kuwa Diamond Platinumz tayari ameanza kushuka kimuziki kama alivyosema awali.
Mtu huyo anayejitambulisha kwa jina la Dr. Yahya Michael ameuambia mtandao wa mamuafrica kuwa kile alichokisema mwanzo kuwa Diamond Platinumz atashuka kimuziki na kurudi pale alipokuwa kimeanza kutokea ingawa watu wengi hawaoni.
“Diamond alikuwa anapiga show kwa milioni 10 lakini sasa hivi hapewi hata show ya milioni 7. Nilizungumza kushuka sio kupanda na nashukuru kwa sababu rekodi ninayo. Nimeongea kushuka sio kupanda, wale walioko nyuma yake hivi sasa ndio wanaonekana kuongoza. Hata katika mambo yenu ya kumi bora za Tanzania yeye hayumo katika mbili.” Amesema Dr. Yahaya

“Sijawahi kumuona mtu anaepanda anaambiwa ameiba nyimbo, sijawahi kuona mtu anaepanda anashindwa na yule ambaye alikuwa anamshinda mwaka jana. Na wala sijawahi kumuona mtu anaeambiwa anapanda halafu anapigwa mawe na watu waliokuwa wanataka wamuone kwa kiingilio kikubwa.” Ameeleza.
USISAHAU KULIKE PAEGE YA FACEBOOK UPATE HABARI ZA HARAKA NA UHAKIKA HAPA>>>>>> MDADISI MAMBO

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger