AMA kweli pombe si maji! Njemba mmoja, Mwala Kibodi a.k.a Chegge (22)
amejikuta akiwa ‘amevurugwa’ na kuzimia mtaroni baada ya kudaiwa kunywa
mizinga minne ya pombe kali aina ya ‘konya’ au ‘ngumu kumeza’.
Tukio hilo la aibu lilijiri Sinza-Lion, Dar wikiendi iliyopita ambapo
Mwala alikutwa na wapita njia waliomtambua kuwa ni fundi makenika
katika gereji moja iliyopo maeneo hayo.
Wakiwa kazini, vijana wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kwa
kushirikiana na raia wema, walianza kumpaka ndimu kama huduma ya kwanza
ambapo hakuonesha kuzinduka hivyo walimpeleka polisi kisha kuchukua fomu
ya matibabu (PF3) na kupelekwa Hospitali ya Sinza-Palestina kwa
matibabu.
Akizungumza na OFM, mmoja wa watu walioshuhudia tukio zima kwa sharti
la kutotajwa jina, alisema Mwala ‘alizima’ kuanzia usiku wa jana yake
mishale ya saa mbili mpaka siku hiyo bila kuzinduka, hali iliyowatia
wasiwasi wakihofia huenda mtu huyo angeweza kupoteza uhai katika maeneo
yao.
Akizungumza na paparazi wetu, rafiki wa karibu wa Mwala, Ramadhan
Tito alisema kuwa awali jamaa huyo alikuwa akibishana na rafiki zake
kwamba anaweza kumaliza mizinga minne ya pombe kali, jambo ambalo
wenzake walimbishia.
Rafiki huyo alitiririka kuwa kwa kuthibitisha kwamba anao uwezo wa
kufanya hivyo, Mwala alizifakamia pombe hizo kwa sifa hadi kuzimaliza.
Rafiki huyo alidai kuwa hadi wanaachana na Mwala usiku ule, hakuwa na
dalili zozote kama asingeweza kufika nyumbani kwake, Mabibo, Dar.
Hadi OFM wanaondoka hospitalini hapo,(usisahau kulike page yetu ya mdadisi mambo blog, bofya hapa)Mwala alikuwa akiendelea na dozi ya kuondoa pombe mwilini. Ulevi noma