Search in This Blog

BAADA YA KUVURUNDA, ABEL DHAIRA APEWA MILION 24 SABABU YA KUVUNJIWA MKATABA WA KE NA KLABU YA SIMBA

 
Abel Dhaira.
IMEELEZWA kuwa, Simba inatakiwa kumlipa kipa wake Abel Dhaira shilingi milioni 24 baada ya uongozi wa timu hiyo kumsitishia mkataba wake.
Kipa huyo amesitishiwa mkataba wake kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa ajili ya kumpisha Yaw Berko anayetarajiwa kusaini hivi karibuni.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo, fedha hizo anazotakiwa kulipwa ni za mwaka mmoja aliobakiza kuichezea Simba.
Chanzo hicho kilisema fedha hizo zinatoka kwenye sehemu ya mshahara wake wa kila mwezi anaoulipwa, ambazo ni milioni mbili, hivyo kwa mwaka ni Sh milioni 24.
“Ili tumalizane na Dhaira, basi tunahitaji tumlipe shilingi milioni 24 baada ya kuusitisha mkataba wake wa kuichezea Simba kwenye usajili huu wa dirisha dogo.
“Fedha hizo ni za malipo yake ya mshahara wa kila mwezi anaolipwa, ambao ni shilingi milioni mbili, hivyo kwa mwaka ni milioni 24 ambazo tunahitaji kumlipa ili tumalizane,” kilisema chanzo hicho.

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger