STRAIKA wa Yanga, Reliants Lusajo, amepanga kurejea
tena shuleni kwa ajili ya kuendelea na masomo yake ya elimu ya juu huku
akiendelea kucheza soka.
Mshambuliaji huyo ambaye ana Shahada ya Ugavi ‘Bachelor of Arts in
Procurement Management ‘aliyoipata kwenye Chuo Kikuu cha Ushirika,
Moshi, alijiunga na Yanga katika usajili mkubwa uliopita.
Lusajo alisema
bado hajaridhika na elimu hiyo aliyoipata, badala yake ataendelea na
masomo ya uzamili ‘masters’ (digrii ya pili).
Lusajo alisema amepanga kusoma masomo ya jioni kwa ajili ya kumpa muda wa kuendelea kuichezea timu hiyo kwenye Ligi Kuu Bara.
“Bado sijaridhika na elimu hii niliyoipata, badala yake nimepanga kuendelea na masomo ili nifikie katika kiwango kizuri.
“Lengo
langu ni kutimiza masters nitakayoipata kwa kusoma masomo ya jioni ili
asubuhi nipate muda wa kufanya mazoezi na wachezaji wenzangu,” alisema
Lusajo.