"MAELEZO YANGU HAYA YATAONDOA UTATA WOTE NA HOPE MTANIELEWA"
1. Ndoa ya kwanza nilichangisha kama UTAMADUNI wa wengi kwenye jamii yetu...
2. Ndoa ya pili.(BOMANI/SERIKALINI)Mungu akanikutanisha na Henry Kilewo
anaejua nini maana ya Mke, anaeniheshimu na kunitunza, anaenipenda na
kunijali.
3.KUMUHUSISHA MUNGU KWENYE TENDO/ KUBARIKI NDOA..
Ningekuwa na mawazo
mgando ningefanya sherehe ya kukata na shoka.. kwanza kutetea jina
langu(umaarufu mavi) na kuwazodoa waliochonga sana kwamba kanisa
nitalisikia kwenye tv na redio na magazeti)
Mimi Joyce Kiria namshukuru Mungu
amenipa Akili za Maisha siyo za darasani za kukopi na kupesti.
Nilizotumia wakati ule ikala kwangu!
HITIMISHO.
Kwa kuwa hatukufanya Sherehe na uwezo tunao, mwakani tutawapeleka Shule
watoto kadhaa wenye uhitaji kwenye jamii yetu. Yule binti aliyeshindwa
kufanya mtihani wa 4m4 kule rombo, tutampeleka private kwa sababu
walisema hawana uwezo huo ndo maana alikuwa tayari kuendelea kusoma
wakati mtoto akiwa na wiki kadhaa toka azaliwe, wale watoto 3 wa Stela
aliyekatwa mkono huko dodoma kama unawakumbuka, watoto 2 wa Gati Chacha
aliyekatwa mguu huko Tarime Mara n.k