Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Bryson
Mwasimba akionbyesha kadi yake ya chama hicho, kabla ya kumkabishi
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto), alipotangaza kuhamia
CCM, leo jioni katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Kata
ya Lupa, wilayani humo.
Bryson Mwasimba kutoka Chadema akikabishi kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
"Sasa Nataka kuungama dhambi nilizowafanyia ndugu zanguni wakati nikiwa
Chadema, Niliwadanganya mengi nanyi mkaniamini. Sasa naungama kwenu
mnisamehe, Lakini mjue kwamba wenye lawama kubwa ni Chadema kwa sera zao
za kuhimiza wanachama na viongozi wake kuwa waongo. Sasa kabla
sijaendelea kusema yaliyo safi naomba kwanza nilivue gwanda hili la
Chadema maana linaninajisi", alisema Bryson, akiwa jukwaani baada ya
kutangaza kuhamia CCM kwenye mkutano huo.
"Sasa ngoja nilivulie mbali hili kwanda nibaki huru", akasema Bryson
wakati akilivua gwanga lake la Chadema, huku akiwa ameshikilia mdomoni
kadi yake mpya ya CCM aliyokabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman
Kinana (kushoto).
Baada ya kulkivua gwanda, Bryson akavaa shati la kijani la CCM.
Kisha akazungumza ya moyoni, huku akimtwisha mzigo wa Lawama Mbunge wa
Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, kwamba amekuwa akimtumbukiza
kwenye madeni mbalimbali kwa kutumia huduma kisha kusepa bila kulipa.
Wakati akisema hayo Nape alikuwa upande wa kulia akimtazama na
kumsikiliza kwa makini sana
Ikawa nderemo na hoi hoi Bryson akabebwa na wana CCM kwa furaha
KABLA YA HAPO KINANA ALIKAGUA UJENZI BARABARA YA CHUNYA HADI TABORA INAYOJENGWA NA KAMPUNI YA CCCC YA CHINA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wasaidizi wake, Katibu wa
NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakikagua sehemu ya ujenzi wa
barabara inayoenda hadi Tabora, unaofanywa na Kampuni ya Kichina ya
CCCC, wakati Kinana na msafara wake walipokuwa wakipita katika eneo
hilo, akiwa njiani kwenda wilayani Chunya, leo
Baadhi ya maeneo yanajengwa kwa uhodari mkubwa kiasi kwamba kupita ni
lazima kuruka, Hapa Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi akiruka kutoka
upande mmoja kwenda mwingine wa eneo hilo linalojengwa.Nyuma yake ni
Kinana ambaye naye alimfuata Nape pia kwa kuruka eneo hilo
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiruka eneo hilo
Kazi ya kuopasuka milima na kuweka sawa inapopita barabara hiyo, ikiendelea
MIKUTANO NA SHUGHULI NYINGINE ZA KINANA WILAYANI CHUNYA
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na
Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwaslimia wananchi,
baada ya msafara wa Kinana kuwasili wilayani Chunya
Kinana akiwasalimia wananchi baada ya kusimamia msafara wake akiwa njiani kwenda Chunya
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua shina la wakereketwa
wajasiriamali wa CCM katika kituo cha mabasi mjini Chunya.
Kisha akakabidhi kazi za CCM kwa wanachama wapya 100 kwenye shina hilo
Kinana akihutubia baada ya kizindua shina hilo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza Kijana, Frank
Mwapololo, ambaye ni mmoja wa wachimbaji wadogo katika machimbo ya
mafunzo kwa ajili ya wachimbaji wadogo, yaliyopo Chunya, alipozungumza
na wajasiriamali wa mradi huo, Nov 30, 2013, akiwa katika ziara kukagua
utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na
kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wapili kulia)
akimrekebishia sawasawa vazi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana,
baada ya wazee wa Kata ya Lupa, wilayani Chunya, kumvalisha vazi la
wazee wa Kata hiyo, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya
chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya
kuzitatua, mkoani Mbeya
Katibu Mkuu wa CCM akiwahutubia wananchi wa Kata ya Lupa,