*Kundi la watu lasambazwa mikoani kumshughulikia
*Mwenyewe akiri kupata taarifa, Chadema yasema ni ratiba ya kawaida
BAADA
ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumvua madaraka
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe, chama hicho sasa
kimechukua hatua ya kusambaza kundi la watu katika mikoa mbalimbali
nchini kwa kazi maalumu ya kushughulika na upepo uliosababishwa na hatua
hiyo.
Habari ambazo zimelifikia Rai Jumapili zinaeleza kuwa
kundi hilo limepewa maelekezo mahususi kutoka makao makuu ya Chadema kwa
ajili ya kwenda kuwashawishi wafuasi na wanachama wake waamini kwamba
kijana huyo ni msaliti.
Kwa mujibu wa habari hizo, kundi hilo la
watu karibu 15 litazunguka mikoani kupeleka kile inachokiita elimu
kuhusu kuvuliwa uongozi kwa Zitto pamoja na Mwanazuoni kutoka katika
Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitila Mkumbo litalenga kuwafikia
wafuasi wa chama hicho hususani vijana kupitia mabaraza yao ya chama
ambao kwao Zitto amekuwa akionekana kama nembo ya mtu anayepigania
mabadiliko.
Source: Mtanzania