Search in This Blog

KOLETHA AFUNGUKA KUHUSU KUCHUKIA WANAUME

Coletha Raymond ‘Koleta’.
MSANII wa maigizo na filamu, Coletha Raymond ‘Koleta’ amefunguka na kutoboa siri ya moyoni juu ya chanzo cha kuwachukia wanaume huku akisisitiza kuendelea kuwa peke yake na kuifanya pombe ndiyo faraja kubwa.  
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu mwanzoni mwa wiki hii, Koleta alisema kamwe hawezi kusahau maumivu aliyopewa na mchumba wake wa zamani baada ya kumfuma zaidi ya mara moja na kumsababishia maumivu makali moyoni.
“Niliumia sana, unajua nilikuwa bado binti hivyo nilimpenda kwa moyo wangu wote, alikuwa akiniambia maneno mengi mazuri na matamu lakini mwisho wa siku nikaishia kuumia,” alisema Koleta.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger