Kutokana
na tukio hilo la kikatili aliofanyiwa bibi huyo kizee aliyefahamika kwa
jina na Bi Asia Mohamed maarufu kwa jina la bibi Chadego, Paparazi wetu
alifika nyumbani kwa bibi huyo mwenye umri wa miaka 65 na kuzungumza na
mjumbe wa eneo hilo bi Hidaya Salum na kusema bibi huyo ameuawa
kikatili akiwa nyumbani kwake huku mtoto wa marehemu naye akieleza
kusikitishwa na kifo cha mama yake.
Baadhi
ya wasamaria wema ambao hawakutaka kutaja majina yao kwa usalama
wao,wamesema bibi huyo alikuwa akihusishwa na mambo ya ushirikina na
baadhi ya familia yake baada ya vifo vya wajukuu wake watatu ambao
walifariki kwa nyakati tofauti kipindi cha nyuma ambao licha ya kudaiwa
wajukuu hao kufariki kwa mambo ya kishirikina lakini ukweli ni kwamba
bibi huyo hakuwa mchawi wala hakuhusika na vifo hivyo huku ikidaiwa
kwamba bibi huyo hakuuawa na mjukuu wake kama inavyodaiwa ila kuna
mchezo uliochezwa na watu fulani ili kumuua na kisha kugeuza kuwa ni
mjukuu wake mwenye tatizo la akili.